Saudi Arabia yakanusha kuishambulia Al-Hudaydah

NA DIRAMAKINI 

MSEMAJI wa Wizara ya Ulinzi ya Saudi Arabia, Brigedia Jenerali Turki bin Saleh Al-Maliki amesema, Taifa hilo halihusiki kwa namna yoyote na shambulizi katika bandari ya Al Hudaydah Magharibi mwa Yemen.
Picha na AA.

Brigedia Jenerali Al-Maliki ameyabainisha hayo baada ya baadhi ya vyombo vya habari ambavyo vinatajwa kuwa ni vya Israel kudai, Saudi Arabia ilihusika na shambulio hilo.

Kwa mujibu wa gazeti la SG, kupitia shambulio hilo la anga jana Jumamosi watu wawili walifariki huku 80 wakijeruhiwa.

Inadaiwa shambulio hilo lilitekelezwa na Israel huku Saudi Arabia ikilitaja kama uchokozi mbaya ambao umelenga miundombinu ya raia nchini Yemen na uhai wa watu.

"Saudi Arabia haina ushiriki au ushirikiano wowote katika kuilenga Al-Hudaydah, na hatutaruhusu uingiliaji wowote wa anga yetu kutoka kwa upande wowote," amesema Brigedia Jenerali Turki Al-Malki, msemaji wa Wizara ya Ulinzi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news