Sekta binafsi ina mchango mkubwa katika maendeleo nchini-Rais Dkt.Mwinyi

DAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Sekta binafsi ina mchango wa kizalendo wa maendeleo wa kuhakikisha Tanzania inazidi kupiga hatua na kwenda sambamba na mabadiliko ya sayansi na teknolojia ili kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi.
Dkt.Mwinyi ameyasema hayo Julai 29,2024 wakati wa Mkutano wa 15 wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Ikulu jijini Dar es Salaam.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amesema maazimio ya mkutano wa 15 wa Baraza la Taifa la Biashara yatakuwa ni dira kutatua changamoto zinazokabili shughuli za biashara nchini na kuwa mwongozo kwa Serikali, watendaji na wafanyabiashara katika kufungua ukurasa mpya wa mageuzi ya kidijiti. Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) kwa umahiri wa uongozi wake wa kukuza uchumi nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news