Serikali kuendelea kutekeleza mapendekezo ya Tume ya Kuboresha Mifumo ya Haki Jinai

KATAVI-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa, Serikali itaendelea kutekeleza mapendekezo ya Tume ya Kuboresha Mifumo ya Haki Jinai ikiwemo kuboresha miundombinu ya Jeshi la Polisi Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akifungua Jengo la Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi.

Rais Dkt. Samia ameyasema hayo wakati akizindua jengo la Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi, ambapo amewataka wananchi kuendeleakutoa ushirikiano kwa Jeshi hilo katika kuhakikisha ulinzi wa raia na mali zao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akifungua Jengo la Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi. Wengine katika picha ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Camillus Wambura pamoja na viongozi wengine leo tarehe 14 Julai, 2024.

Wakati akizindua ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa vya kuhifadhi nafaka, Rais Dkt. Samia ameielekeza Wakala wa Taifa wa
Hifadhi ya Chakula kuufanya Mkoa wa Katavi kuwa kanda inayojitegemea kwenye ununuzi na uhifadhi wa nafaka.
Mradi huo ambao utasaidia kukabiliana na usalama wa chakula na kupunguza upotevu wa chakula baada ya kuvunwa, umeongeza uwezo wa Mkoa wa Katavi kuhifadhi nafaka kutoka tani 5,000 hadi tani 28,000.

Aidha, kufuatia msimu mpya wa ununuzi wa nafaka kuzinduliwa, Rais Dkt. Samia amesisitiza umuhimu wa wanunuzi wa mazao kote nchini kuzingatia haki wakati waununuzi
na kutoa bei nzuri kwa wakulima.
Rais Dkt. Samia pia ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali yaRufaa ya Mkoa wa Katavi ambao ni sehemu ya uimarishaji wa huduma za afya zinazotolewa katika Hospitali za Rufaa za Mikoa 28 nchini, ikiwemo huduma zamama na mtoto.
Halikadhalika, Rais Dkt. Samia amewahimiza wananchi mkoani humo kushirikiana na Serikali kudhibiti mimba za utotoni na kuhakikisha watoto wa kike wanapata
fursa ya kupata elimu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news