Serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wafadhili na wawekezaji nchini

MANYARA-Mahusiano mazuri yaliyowekwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan yameendelea kuonekana kwa vitendo.
Hayo yamesemwa Julai 6, 2024 na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini, Mhe. Daniel Sillo wakati akizungumza na wananchi wa Kata za Arri na Ayalagaya kwenye hafla ya kuwaaga wadau wa maendeleo Taasisi ya Karim Foundation waliofika nchini hapa kwa mapumziko ya wiki mbili.
Mhe. Sillo amesema nchi itaendelea kudumisha amani na utulivu uliopo ili wawekezaji na wafadhili mbalimbali wafanye kazi zao bila hofu, hivyo amempongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuifungua nchi, kuwavutia wawekezaji, kudumisha ulinzi na usalama na kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta zote.

"Nchi kama haipo salama huwezi kupata wafadhili kama hawa na kuwekeza pesa nyingi kiasi hiki."

Aidha,Mhe. Sillo amewaomba wakazi wa maeneo hayo ambayo yupo Mfadhili huyo waendelee kuboresha mahusiano mazuri yaliyopo ili aendelee kuwepo pia kuendelea kutunza miradi yote ambayo imeletwa katika maeneo yao.
Naye Mkurugenzi wa Kimataifa wa Taasisi ya Karim Foundation, Nelson Mattos amesema, ataendelea kutoa fedha kutoka kwa wadau wake lengo likiwa kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Babati Vijijini, Jackson Hhaibey amewapongeza wadau hao kwa kuendelea kuiunga mkono Serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo iliyonadiwa kwenye Ilani ya Chama chake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news