RUVUMA-Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu),Mhe. Jenista Mhagama ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho ameelekeza Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma kuhakikisha Daraja la Lumecha linajengwa ndani ya kipindi kifupi na kwa ubora.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akizungumza na wananchi wa Liweta katika mkutano wa hadhara kuhusu ujenzi wa Daraja la Lumecha unatarajia kuanza hivi karibuni.
Waziri ametoa kauli hiyo Julai 10,2024 wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi ya maendeleo katika Kijiji cha Liweta Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.



“Serikali imetoa kiasi cha shilingi milioni 400 kujenga madaraja na akiba ya fedha itakayobaki itatumika kutengeneza barabara mpaka Kijiji cha Liweta ikiwa ni pamoja na kufukia shimo lilopo katika barabara hiyo."
Amesema, kazi ya ujenzi wa barabara ni kazi muhimu, "naomba wananchi msaidie katika kulinda mradi ili ujenzi ukamilike kwa wakati na tufungue njia zitakazochochea uchumi katika Kijiji cha Liweta."