Serikali yatoa taarifa njema kwa wakulima

RUVUMA-Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Jenista Mhagama ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho ameomba wananchi kuanza kujiandaa ili kulifanya zao la mahindi kuwa zao la biashara kwa siku za usoni.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho akizungumza na Wazee wa Kijiji cha Kikunja wakati alipotembelea na kufanya mkutano wa hadhara.

Waziri ametoa kauli hiyo Julai 8,2024 katika ziara yake katika Kata ya Matimila ambapo amefanya mikutano miwili ya hadhara katika vijiji vya Kikunja na Mpingi vilivyopo Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.
Mhe. Bahati Kambi Diwani wa Viti Maalum akisalimia Wananchi katika Kijiji cha Mpingi wakati wa Mkutano wa hadhara wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb).

Amesema, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu ameendelea kutoa ruzuku ya mbolea, "kazi kubwa kwetu wakulima ni kuongeza juhudi katika kilimo na uzalishaji wa mahindi.
Wananchi wa Mpingi na Kikunja wakimsikilza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho katika Mkutano wa Hadhara alioufanya katika kijiji hicho.

"Mwaka huu Mheshimiwa Rais, ametutafutia masoko nje ya nchi, lengo letu ni kuhakikisha siku za karibuni tunafanya zao la mahindi kuwa zao la biashara ili liweze kusaidia wananchi kukuza uchumi na pato la familia.”

Aidha,Waziri amewaomba wananchi kuendelea kuweka akiba ya chakula cha familia badala ya kuuza chakula chote ili nchi iendelee kuwa na akiba ya chakula.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho akizungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara aliyofanya katika kijiji cha Kikunja na Mpingi Kata ya Matimila.

Waziri ameelezea wananchi kuhusu fursa ya mikopo yenye masharti nafuu, ambapo amewaasa kutumia wasaa huo kufungua shughuli mbalimbali za uchumi, ikiwemo mashine za kusaga za umeme, na kujikita katika kuwekeza katika viwanda vidogo vidogo vya kuchoma chuma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho akipokea kadi na kumkaribisha na Ndg. Joseph Lufunda mwanachama mpya wa CCM aliyehamia kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo.

“Nishati ya umeme inatakiwa kuwasaidia wananchi kupata mapato na shunguli za kukuza kiuchumi,” amesema Waziri Mhagama.

Awali Katibu Tawala wa Wilaya ya Songea, Mtela Mwapamba amewaambia wananchi kwamba watafanya mikutano ya ujirani mwema kati ya Mkuu wa Wilaya ya Songea na Wilaya ya Namtumbo na Kamati za ulinzi na Usalama ili kutatua migogoro ya Mipaka inayohusianisha wilaya hizo mbili.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho akiteta jambo na Katibu Tawala wa Wilaya ya Songea,Mtela Mwapamba wakati wa Mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kikunja.

Aidha, Katibu Tawala amewaahidi wananchi wa Kijiji cha Kikunja kwamba Serikali kupitia Afisa Ushirika wa Halmashauri ya Songea , itawasaidia kuanzishwa kwa chama chao cha Ushirika katika Kijiji hicho ambacho hakina (AMCOS) Agricultural Marketing Cooperative Society.

“Kuanzishwa kwa AMCOS itasaidia Serikali kupata mapato hivyo ni jukumu la Watendaji wa Serikali kuhakikisha inasimamia mchakato na kanuni za uanzishwaji wake tangu mwanzoni mpaka ukamilikaji wake na kuhakikisha tunailea,“amesema Mwapamba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news