Sillo afanya Mkutano wa 93 kati ya Vijiji 102

MANYARA-Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Daniel Sillo amefanya Mkutano wa hadhara katika Vijiji vya Endakiso na Arri na kusikiliza kero mbalimbali za Wananchi ikiwa ni Mkutano wake wa 93 kati ya Vijiji 102 kwenye kata 25 za Jimbo la Babati Vijijini.
Mhe. Sillo amesema kwa Kipindi cha Miaka Mitatu pekee Serikali imejenga Zahanati 9 kila moja ikigharimu Shilingi Milioni 50, ambavyo kwa sasa zinatoa huduma kwa Wananchi.
"Kwenye Mikutano yangu nataja vitu vilivyofanyika ambavyo Wananchi wanaviona kwa macho na sio kutukana kama wenzetu wanavyofanya."

Vilevile amesema kwenye Kata ya Arri pekee zimetolewa Shilingi Milioni 424 zilizoelekezwa kwenye miradi ya maendeleo ya afya na elimu na Kata ya Endakiso zaidi ya Shilingi Milioni 200.
Amesema Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ndio ina mkataba na wananchi hivyo atahakikisha anashirikiana na chama pamoja na Serikali kuwaletea wananchi maendeleo.

Ametaja miradi mikubwa ya Kitaifa inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ikiwa ni pamoja na Mradi wa Kufua Umeme wa Bwawa la Mwalimu Nyerere itakayosaidia Wananchi kupata Nishati ya uhakika ambayo itasaidia kukuza Uchumi pamoja na Reli ya Kisasa ya Umeme (SGR) inayokwenda maeneo mbalimbali nchini hivyo kurahisisha usafirishaji bidhaa kutoka eneo moja kwenda lingine.

Aidha,amewakumbusha Wananchi wenye sifa za kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi kujitokeze katika kugombea nafasi kwenye uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji.
Pia katika ziara yake Mhe. Sillo ameambatana na Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Babati ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Ndg. Jackson Hhaibey.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news