LUSAKA-Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Daniel Sillo (Mb) leo Julai 12, 2024 Jijini Lusaka, Zambia ameshiriki mazungumzo yaliyofanywa kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Africa Mashariki, Mhe. January Makamba na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Mhe. Elias Mpedi Magosi.


