KAGERA-Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Daniel Sillo (Mb) amewasili Wilayani Ngara Mkoani Kagera kufanya ziara ya kikazi ambapo amepokelewa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ngara Bi. Hatujuani Lukari kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya leo Julai 29, 2024.

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri Sillo atapokea taarifa ya hali ya usalama Wilayani humo, atakagua eneo la Shamba la Jeshi la Magereza pamoja na kufanya mkutano wa hadhara.
Mbunge Ndaisaba amemshukuru Naibu Waziri Sillo kwa kutimiza ahadi yake ya kufanya ziara katika Jimbo hilo.