DAR-Aliyekuwa mwigizaji na msanii wa Muziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania, Snura Anton Mushi ametangaza kuacha muziki rasmi.
Badala yake mwana mama huyo amesema ataendelea kumcha Mungu baada ya kufanya kazi hiyo kwa miaka kadhaa.
Ameyabainisha hayo Julai 29,2024 kwa madai kuwa, hatamani kuona watoto wake wakisema mama ni msanii na ameitikia ushauri wa mume wake.