Spika Dkt.Tulia amuapisha Balozi Kombo kuwa Mbunge, amuuma sikio

DAR-Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Akson amemtaka Mbunge mteule, Balozi Mahmoud Thabit Kombo kumsaidia Rais katika kuhakikisha wanaendeleza mahusiano kati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kimataifa.Amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan anatekeleza mipango mingi hivyo, wana jukumu la kumsaidia katika kutekeleza mipango hiyo kama alivyowaamini.
Dkt. Tulia ameyasema hayo leo katika Ofisi ndogo za Bunge zilizopo Dar es Salaam baada ya kumwapisha Balozi Kombo kuwa Mbunge ambaye aliteuliwa na Rais Samia kuwa Mbunge na Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Julai 21, mwaka huu.

Spika amempongeza Balozi Kombo kwa kuaminiwa na Rais katika nafasi hiyo ya ubunge kwamba nafasi hizo ni chache na kuwepo miongoni mwao ni heshima kubwa.
Amemtaka Mbunge huyo kufanya kazi kwa ushirikiano kuhakikisha taifa linasonga mbele na kufanyia kazi mipango ya Rais na kwamba wanatarajia wao wataendeleza mipango hiyo ya mahusiano ya Afrika Mashariki na kimataifa.

"Tunaamini mtaendelea kushirikiana kuhakikisha gurudumu la maendeleo ya nchi hii linaendelea kusonga mbele," amesisitiza Dkt. Tulia.
Amesema kuwa, Balozi Kombo ameapa kiapo cha uaminifu ambacho kinamfanya kuwa Mbunge kwa matakwa ya Ibara ya 68 ya Katiba na Kanuni ya 30 fasili ya kwanza ambayo inaeleza kabla ya mbunge kushiriki shughuli za bunge, lazima awe amekula kiapo cha uaminifu mbele ya Spika.

Pia ameeleza sababu ya kumwapishia Dar es Salaam kwamba fasili ndogo ya (2) (b) ya kanuni za bunge ambazo zimefanyiwa marekwbisho, inaeleza kuwa Mbunge ataapishwa na Spika kiapo cha uaminifu eneo litakalopangwa na Spika.
"Kanuni zinaruhusu mbunge kuapishwa popote pale ambapo Spika ameagiza ikiwa ni nje ya bunge au bungeni. Leo tumefanyia Dar es Salaam lakini tungeweza kufanya sehemu nyingine yoyote na kanuni zetu zinaruhusu," amesisitiza.
Baadhi ya wabunge walioshiriki katika hafla hiyo ni Stegomena Tax Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Londo ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news