Tamasha la Mwaka Kogwa ni fursa kwa wananchi-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema,Tamasha la Mwaka Kogwa ni fursa kwa wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja kuimarisha utalii wa ndani na wa Kimataifa. Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo leo Julai 16,2024 katika tamasha hilo lililofanyika uwanja wa Kae Kuu, Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja.
Aidha,Rais Dkt.Mwinyi ametoa wito kwa uongozi wa Mkoa na Wilaya kuwa na mipango mizuri ya kuhakikisha matamasha yanaleta manufaa kwa kutoa fursa mbalimbali za maendeleo zinazoambatana na matukio ikiwemo michezo ya asili na miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuyaimarisha matamasha yaliyopo na kubuni mapya kwa lengo la kuongeza vivutio vya utalii nchini na kudumisha mila, desturi na utamaduni wa Mzanzibari.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news