Tanzania ipo mbioni kujitosheleza kwa mbolea-Dkt.Diallo

DAR-Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imesema kuwa, uzalishaji wa ndani wa mbolea utaongezeka ifikapo mwishoni mwa mwaka huu na hivyo kutosheleza mahitaji ya soko ya pembejeo hiyo muhimu.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Dkt. Antony Diallo jijini Dar es Salaam, alipotembelea banda la Mamlaka kwenye Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara maarufu Sabasaba yanayoendelea.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Dkt. Anthony Diallo akiwasili katika viwanja vya maonesho ya Biashara ya Kimataifa - sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. Julius K. Nyerere Jijini Dar Es Salaam tarehe 11 Julai, 2024.

Dkt. Diallo amesema, Agenda 10/30: Kilimo ni biashara inatutaka ifikapo mwaka 2030 Tanzania iwe na uwezo wa kujitosheleza kwa mbolea pamoja na kuuza nchi jirani kutokana na uwepo wa viwanda vinavyotosheleza mahitaji ya nchi.
"Siyo tu kusubiri mwaka 2030 kwa sasa tumeshaanza kuzalisha kiwango kikubwa cha mbolea nchini na tunatarajia hadi mwisho wa mwaka huu (2024) tutakuwa na uwezo wa kuzalisha kiwango chote cha mahitaji yetu," Dkt. Diallo alisema.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamalaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Dkt. Anthony Diallo akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Mamlaka katika maonesho ya Sabasaba yanayoendelea Jijini Dar Es Salaam tarehe 11 Julai, 2024.

Alisema, kwa sasa upatikanaji wa mbolea nchini unafikia asilimia 80 hadi 90 na kwamba mahitaji ni takribani tani 850,000 na yanaelekea kufikia tani milioni moja ambazo zinaweza kuzalishwa nchini.
Mwenyekiti wa Bodi ya TFRA, Dkt. Anthony Diallo (kushoto) akimhoji mwoneshaji wa Mamlaka kwenye maonesho ya Biashara ya Kimataifa John Sostheness alipotembelea banda hilo tarehe 11 Julai, 2024.

Amesema, fursa za kuwekeza nchini ni nyingi zinazoendana na upatikanaji wa malighafi zinazoweza kutumika kuzalisha mbolea nchini.

Kufuatia hilo, ni vyema Mamlaka kutangaza fursa hizo muhimu ili kupata wawekezaji watakaowekeza kwenye viwanda vya mbolea na hivyo kuisaidia nchi kuondokana na utegemezi.
Mwenyekiti wa Bodi ya TFRA, Dkt. Anthony Diallo (katikati) akiwa katika picha na watumishi wa Mamlaka wanaotoa elimu ya mbolea kwa watembeaji wa maonesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. J. K. Nyerere jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa huduma za Mamlaka, Victoria Elangwa.

Dkt. Diallo amesema maonesho hayo ni muhimu kwasababu watu kutoka mataifa mengine wanafika na hivyo kutupa fursa ya kupata wanunuzi wa mbolea zinazozalishwa Tanzania.
Mwenyekiti wa Bodi ya TFRA, Dkt. Anthony Diallo (katikati) akiwa katika picha na watumishi wa Mamlaka wanaotoa elimu ya mbolea kwa watembeaji wa maonesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. J. K. Nyerere jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa huduma za Mamlaka, Victoria Elangwa.

Mwisho, Dkt. Diallo ametoa wito kwa Watanzania kutembelea banda hilo ili kupata elimu ya shughuli zinazosimamiwa na Mamlaka kwa maslahi ya sekta ya kilimo na Taifa kwa ujumla.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news