VICTORIA FALLS-Tanzania inatarajiwa kuwa Mwenyeji wa Kongamano la Pili la Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UN Tourism), Kanda ya Afrika kuhusu utalii wa vyakula vya asili katika Bara la Afrika kwa mwaka 20.
Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe, Mhe. Emmerson Mnangagwa (katikati) akiwa ameongozana na Mke wake, Dkt. Auxillia Mnangagwa (kushoto) kukagua mabanda ya maonesho ya vyakula kwenye Kongamano la kwanza la Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani, Kanda ya Afrika kuhusu Utalii wa vyakula vya asili katika Bara la Africa (Gastronomy) jijini Victoria Falls nchini Zimbabwe Julai 26, 2024. Wengine pichani ni Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UN Tourism), Zurab Pololikashvili, Wake wa Marais wa Serbia, Angola, baadhi ya Mawaziri kutoka nchi za Afrika pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Zimbabwe.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UN Tourism), Zurab Pololikashvili katika ufunguzi wa Kongamano la kwanza la Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani, Kanda ya Afrika kuhusu Utalii wa vyakula vya asili katika Bara la Africa (Gastronomy) linaloendelea jijini Victoria Falls nchini Zimbabwe tarehe 26 Julai, 2024.
Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UN Tourism), Zurab Pololikashvili akizungumza katika ufunguzi wa Kongamano la kwanza la Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani, Kanda ya Afrika kuhusu Utalii wa vyakula vya asili katika Bara la Africa (Gastronomy) jijini Victoria Falls nchini Zimbabwe Julai 26, 2024.
Bw. Pololikashvili amemshukuru Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania, Mhe. Angellah Kairuki kwa ushirikiano wake na nia yake ya kutaka kutangaza utalii wa chakula na kusisitiza kuwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani liko tayari kutoa ushirikiano kwa nchi za Afrika katika kutangaza utamaduni wa Kiafrika hasa Utalii wa vyakula.
"Afrika sio tu kwa ajili ya safari na kuangalia mazingira ya asili, bali pia tunataka kuuonesha ulimwengu kwamba Afrika ni tajiri katika utamaduni hasa utalii wa vyakula ambao ni sehemu kubwa ya utamaduni wetu," alisisitiza.
Naye, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) amesema kufanyika kwa Kongamano hilo nchini Tanzania kutakuwa na manufaa makubwa katika kukuza mnyororo mzima wa thamani katika utalii ikiwemo Utalii wa vyakula hasa kugusa wadau wengi wakiwemo wakulima wafugaji, wavuvi,wazalishaji wa nafaka, wachakataji wa mafuta n.k.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) katika ufunguzi wa Kongamano la kwanza la Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani, Kanda ya Afrika kuhusu Utalii wa vyakula vya asili katika Bara la Africa (Gastronomy) jijini Victoria Falls nchini Zimbabwe Julai 26, 2024.
Ujumbe wa Tanzania ulishiriki ufunguzi wa Kongamano la kwanza la Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani, Kanda ya Afrika kuhusu Utalii wa vyakula vya asili katika Bara la Africa (Gastronomy) jijini Victoria Falls nchini Zimbabwe Julai 26, 2024. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Utawala, Ubalozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Bi. Gwantwa Mwaisaka, Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT), Dkt. Florian Mtey, Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Tafiti na Ushauri, Jesca William na Afisa Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Matatizo Kastamu.
"Tunao mwaka mmoja wa kufanya maandalizi na tutajipanga vizuri kuhakikisha kwamba Tanzania inaonesha urithi na utajiri mkubwa tulionao lakini ni nafasi nzuri katika kukuza utalii wetu zaidi," Mhe. Kairuki ameongeza.
Amefafanua kuwa, kupitia jukwaa hilo kutakuwa na mashindano mbalimbali kwa ajili ya ubunifu na wenye vyuo na wataalamu wengine watapata nafasi ya kubadilishana uzoefu na wenzao kutoka nchi nyingine za Afrika.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (katikati) katika picha ya pamoja na Mkuu wa Utawala, Ubalozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Bi. Gwantwa Mwaisaka (wa pili kutoka kushoto), Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT), Dkt. Florian Mtey (wa pili kutoka kulia) , Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Tafiti na Ushauri, Jesca William (kushoto) na Afisa Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Matatizo Kastamu (kulia).
Kongamano hilo limefunguliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe, Mhe. Emmerson Mnangagwa ambaye amesisitiza juu ya umuhimu wa Sekta ya Kilimo katika kukuza Utalii wa Chakula.