Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Pili wa Wahasibu barani Afrika (AAAG)

PETER HAULE NA
JOSEPH MAHUMI

TANZANIA inatarajia kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Pili wa Wahasibu Barani Afrika (African Association of Accountants General Meeting (AAAG)) utakaofanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 3 hadi 5 Disemba Mwaka 2024, ukiwahusisha zaidi wa washiriki 2,000 kutoka takriban nchi 55 za Bara la Afrika.
Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA Leonard Mkude (kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala Wizara ya Fedha, Bw. Renatus Msangira, wakiteta jambo wakati wanawasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), kufanya Mkutano na wanahabari, kuhusu ujio wa Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Wahasibu Wakuu wa nchi za Afrika (African Association of Accountants General-AAG Meeting) unaotarajiwa kufanyika tarehe 3 hadi 5 Disemba Mwaka huu, katika Kituo hicho, ambapo wamewaeleza wanahabari kuwa mkutano huo unatarajia kuleta manufaa makubwa kiuchumi na kijamii pamoja na kuitangaza sekta ya utalii ya Tanzania, kwa wajumbe kutembelea vivutio vya utalii hususan vilivyoko katika ukanda wa Kaskazini.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Arusha).

Hayo yameelezwa na Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA Leonard Mkude, wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari jijini Arusha, uliolenga kuujulisha umma kuhusu mkutano huo na fursa za kiuchumi na kijamii kwa watanzania.

CPA Mkude alisema kuwa mkutano huo unatarajia kuleta manufaa makubwa kiuchumi na kijamii pamoja na kuitangaza sekta ya utalii ya Tanzania, hususan kwa wajumbe kutembelea vivutio vya utalii vilivyoko katika ukanda wa Kaskazini.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja, akiongoza Mkutano wanahabari katika ukumbi wa Mikutano katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), kuhusu ujio wa Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Wahasibu Wakuu wa nchi za Afrika (African Association of Accountants General-AAG Meeting) unaotarajiwa kufanyika tarehe 3 hadi 5 Disemba Mwaka huu, katika Kituo hicho cha AICC, ambapo Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA Leonard Mkude, Mwenyekiti wa Umoja wa Wahasibu wa Afrika, ambaye pia ni Mhasibu Mkuu wa Serikali ya Lesotho, Bi. Malehlohonolo Mahase na Mkurugenzi Mkuu wa AICC, Bi. Christine Mwakatobe, wamewaeleza wanahabari kuwa mkutano huo unatarajia kuleta manufaa makubwa kiuchumi na kijamii pamoja na kuitangaza sekta ya utalii ya Tanzania, kwa wajumbe kutembelea vivutio vya utalii, hususan vilivyoko katika ukanda wa Kaskazini.

Alizitaja faida nyingine za mkutano huo kuwa ni pamoja na kuwa na Afrika yenye mafanikio yenye msingi wa ukuaji jumuishi na maendeleo endelevu, Bara jumuishi lililounganishwa kisiasa na kwa kuzingatia maadili ya Pan-Africanism.

Aliyataja manufaa mengine kuwa ni pamoja na kuwa na maono ya Mwamko wa Afrika na Afrika yenye utawala bora, demokrasia, kuheshimu haki za binadamu na utawala wa sheria, Afrika yenye amani na usalama na Afrika yenye utambulisho thabiti wa kitamaduni, urithi wa pamoja na maadili.
Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA. Leonard Mkude (Katikati), akizungumza na wanahabari katika ukumbi wa Mikutano katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), kuhusu ujio wa Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Wahasibu Wakuu wa nchi za Afrika (African Association of Accountants General-AAG Meeting) unaotarajiwa kufanyika tarehe 3 hadi 5 Disemba Mwaka huu, katika Kituo hicho , ambapo washiriki zaidi ya 2,000 kutoka nchi za Afrika na unalenga kujenga Imani ya umma katika Mifumo ya Usimamizi wa Fedha za Umma kwa Ukuaji Endelevu. Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wahasibu Wakuu wa Afrika, Bi. Malehlohonolo Mahase, na Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), Bi. Christine Mwakatobe.

CPA Mkude alisema kuwa Mkutano huo utawaleta Wahasibu wakuu wa Serikali Afrika watakaoambatana na Wahasibu Wakuu wa Wizara, Taasisi za umma na Wahasibu na wadau wengine ambao watapata fursa ya kusikiliza mada za masuala mbalimbali ya kitaaluma na kubadirishana mawazo na kujua fursa zinazopatikana katika nchi za Afrika.

Alisema wageni kutoka nje watakuja na fedha za kigeni ambazo watazitumia hapa Tanzania kwa kuwa watatembezwa kwenye mbuga za Wanyama na vituo mbalimbali vya utalii na hivyo kuunga mkono dhamira ya Mheshimiwa Rais ya kuutangaza Utalii wa Tanzania.
Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA. Leonard Mkude, akizungumza na wanahabari katika ukumbi wa Mikutano katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), kuhusu ujio wa Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Wahasibu Wakuu wa nchi za Afrika (African Association of Accountants General-AAG Meeting), unaotarajiwa kufanyika tarehe 3 hadi 5 Disemba Mwaka huu, katika Kituo hicho cha AICC, na utawashirikisha zaidi ya washiriki 2,000 kutoka nchi za Afrika na mkutano huo unalenga kujenga Imani ya umma katika Mifumo ya Usimamizi wa Fedha za Umma kwa Ukuaji Endelevu.

Alitoa wito kwa wafanyabiashara wa nyumba za wageni (hoteli), usafiri, mamalishe na jamii kwa ujumla kuchangamkia fursa hiyo ya ujio wa wageni ili kunufaika kiuchumi na kijamii.

“Natoa wito kwa Maafisa Masuuli wa Wizara na Taasisi zote kuwaruhusu Wahasibu, wakaguzi na wadau wengine watakaoomba kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Pili wa Wahasibu wakuu wa Serikali Afrika, African Association of Accountants General (AAAG) utakaofanyika jijini Arusha mwezi Desemba, 2024”, alisema CPA Mkude.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wahasibu Wakuu wa Afrika ambaye pia ni Mhasibu Mkuu wa Serikali ya Lesotho, Bi. Malehlohonolo Mahase, akizungumza wakati wa Mkutano na wanahabari katika ukumbi wa Mikutano katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), kuhusu ujio wa Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Wahasibu Wakuu wa nchi za Afrika (African Association of Accountants General-AAG Meeting) unaotarajiwa kufanyika tarehe 3 hadi 5 Disemba Mwaka huu, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), ambapo amesema kuwa Mkutano huo utakawakutanisha pia Jumuiya za wafanyabiashara na watapa fursa ya kujua ni namna gani Afrika ipo tayari katika suala la uwekezaji na namna ya kuripoti hali ya Uchumi ya Afrika, jambo ambalo litaongeza uwazi na uwajibikaji.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Wahasibu wa Afrika, ambaye pia ni Mhasibu Mkuu wa nchi ya Lesotho, Bi. Malehlohonolo Mahase, alisema Mkutano wa Wahasibu Afrika unafanyika Tanzania kwa kuwa ni mwanachama anayeaminika na amekuwa mshiriki mwaminifu katika umoja huo, na kwamba wajumbe wa mkutano huo wanakuja kujifunza namna Tanzania ilivyopiga hatua kubwa katika matumizi ya mifumo ya fedha.
Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala Wizara ya Fedha, Bw. Renatus Msangira (Kulia) na Mhasibu Mkuu Msaidizi wa Serikali, Bw. Victus P. Tesha, wakifuatilia Mkutano na wanahabari katika ukumbi wa Mikutano katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), kuhusu ujio wa Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Wahasibu Wakuu wa nchi za Afrika (African Association of Accountants General-AAG Meeting) unaotarajiwa kufanyika tarehe 3 hadi 5 Disemba Mwaka huu, katika Kituo hicho cha AICC, ambapo Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA Leonard Mkude, Mwenyekiti wa Umoja wa Wahasibu wa Afrika, ambaye pia ni Mhasibu Mkuu wa Serikali ya Lesotho, Bi. Malehlohonolo Mahase na Mkurugenzi Mkuu wa AICC, Bi. Christine Mwakatobe, wamewaleza wanahabari kuwa mkutano huo unatarajia kuleta manufaa makubwa kiuchumi na kijamii pamoja na kuitangaza sekta ya utalii ya Tanzania, hususan kwa wajumbe kutembelea vivutio vya utalii vilivyoko katika ukanda wa Kaskazini.

Alisema kuwa Tanzania ipo vizuri katika kutekeleza viwango vya kimataifa vya kihasibu, imekuwa ya mfano katika ukuaji wa Uchumi, imeimarika katika suala la ukarimu wa wageni, maendeleo katika teknolojia ya Habari na Mawasiliano na ni miongoni mwa nchi zenye vivutio vingi vya utalii hivyo wanachama kuna mambo mengi ya kujifunza.

Aidha alieleza kuwa Mkutano huo utakao wakutanisha pia Jumuiya za wafanyabiashara watapata fursa ya kujua ni namna gani Afrika ipo tayari katika suala la uwekezaji na namna ya kuripoti hali ya Uchumi ya Afrika, jambo ambalo litaongeza uwazi na uwajibikaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), Bi. Christine Mwakatobe, akizungumza kuhusu fursa ambazo Tanzania na wakazi wa mkoa wa Arusha watapata wakati wa Mkutano na wanahabari katika ukumbi wa Mikutano katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), kuhusu ujio wa Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Wahasibu Wakuu wa nchi za Afrika (African Association of Accountants General-AAG Meeting) unaotarajiwa kufanyika tarehe 3 hadi 5 Disemba Mwaka huu, katika Kituo cha AICC, ambapo amesema kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha wageni wanapokuja wanapata huduma bora na watakua mabalozi wazuri wa Tanzania.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Bi. Christine Mwakatobe alisema kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha wageni wanapokuja wanapata huduma bora kwa kuwa wanaamini watakuwa mabalozi wa Tanzania na watatembelea vivutio mbalimbali vya utalii.
Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA Leonard Mkude (Katikati), Mwenyekiti wa Umoja wa Wahasibu wa Afrika, ambaye pia ni Mhasibu Mkuu wa nchi ya Lesotho, Bi. Malehlohonolo Mahase (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Mikutano wa Kitamaifa (AICC), Bi. Christine Mwakatobe, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Mkutano wao na wanahabari katika ukumbi wa Mikutano katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), kuhusu ujio wa Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Wahasibu Wakuu wa nchi za Afrika (African Association of Accountants General-AAG Meeting) unaotarajiwa kufanyika tarehe 3 hadi 5 Disemba Mwaka huu, katika Kituo hicho, ambapo wamewaeleza wanahabari kuwa mkutano huo unatarajia kuleta manufaa makubwa kiuchumi na kijamii pamoja na kuitangaza sekta ya utalii ya Tanzania, kwa wajumbe kutembelea vivutio vya utalii hususan vilivyoko katika ukanda wa Kaskazini.

Alisema anamshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuitangaza nchi yetu Duniani na kwamba hauo ni matunda ambayo Taasisi za Serikali kwa ujumla zinafaidi kwa kazi yake anayoifanya, huku Kituo chake cha Mikutano kikihudumia mikutano mingi ya Kitaifa na Kimataifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news