ADDIS SABABA-Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, ameongoza Ujumbe wa Tanzania kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) katika Kikao cha Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Nne wa Kimataifa wa Ugharamiaji kwa Maendeleo Endelevu (Fouth International Conference on Financing for Development - FfD4), kinachofanyika jijini Addis Ababa nchini Ethiopia, ambapo nchi mbalimbali zimekutana kujadiliana namna ya kukuza uchumi wa nchi zao.