Tanzania yasisitiza umuhimu wa takwimu kiuchumi

NA ASIA SINGANO
WF Ethiopia

SERIKALI ya Tanzania imeushauri Umoja wa Mataifa kuanzisha mfumo thabiti wa takwimu utakaosaidia kupata taarifa sahihi kuhusu masuala ya uchumi kuelekea azimio la Ajenda ya Hatua ya Addis Ababa.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, akiwasilisha hoja mbalimbali wakati wa kufunga Kikao cha Kwanza cha Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Nne wa Kimataifa wa Ugharamiaji kwa Maendeleo Endelevu (Fouth International Conference on Financing for Deveoplopment - FfD4, kilichofanyika mjini Addis Ababa nchini Ethiopia, lengo likiwa ni kuandaa mkutano huo unaotarajiwa kufanyika mwakani.

Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, mjini Addis Ababa nchini Ethiopia, kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), wakati wa kufunga kikao cha kwanza cha Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Nne wa Kimataifa wa Ugharamiaji kwa Maendeleo Endelevu (Fouth International Conference on Financing for Deveoplopment - FfD4 unaotarajiwa kufanyika mwakani.

Alisema kuwa mfumo huo wa takwimu utasaidia kupata taarifa sahihi na kwakuwa upatikanaji wa takwimu hizo ni muhimu hasa kwa nchi zinazoendelea kama Tanzania katika kusaidia ukuaji wa uchumi jumuishi.

“Takwimu zitaongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wetu wa kushughulikia changamoto za maendeleo kama vile umaskini, ukosefu wa usawa, mabadiliko ya hali ya hewa, masuala ya mazingira, amani, na haki,” alisema Bi. Amina.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Mhe. Innocent Shiyo, mara baada ya kufika katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia, pamoja na ujumbe wa Tanzania baada ya kumalizika Kikao cha Kwanza cha Maandalizi ya Mkutano wa Nne wa Kimataifa wa Ugharamiaji kwa Maendeleo Endelevu (Fouth International Conference on Financing for Deveoplopment - FfD4, kilichofanyika mjini Addis Ababa nchini humo.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Mhe. Balozi Innocent Shiyo baada ya ujumbe huo wa Tanzania kutembelea Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia baada ya kumaliza kikao cha kwanza cha Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Nne wa Kimataifa wa Ugharamiaji kwa Maendeleo Endelevu (Fouth International Conference on Financing for Deveoplopment - FfD4, kilichofanyika mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Katika hatua nyingine Bi. Amina ameushauri Umoja wa Mataifa kuwekeza katika mawazo ya ubunifu ili kusaidia nchi zinazoendelea katika kutumia teknolojia mpya za data, kutumia data iliyogawanywa kijinsia katika ufadhili wa maendeleo ili kutambua na kushughulikia usawa wa kijinsia.

Aliongeza kuwa ni vyema Umoja wa Mataifa itambue hitaji la njia kamili ambayo inaenea zaidi ya vipimo vya Pato la Taifa katika kutathmini maendeleo ya kitaifa na kutetea kupitishwa kwa viashiria vya pande nyingi.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban (katikati) akimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Mhe. Innocent Shiyo (wakwanza kushoto), pamoja na Kamishna Msaidizi, kutoka Wizara ya Fedha, Idara ya Fedha za Nje, Bw. Patrick Pima, katika Ofisi ya Balozi huyo nchini Ethiopia walipomtembelea mara baada ya kumalizika kwa Kikao cha Kwanza cha Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Nne wa Kimataifa wa Ugharamiaji kwa Maendeleo Endelevu (Fouth International Conference on Financing for Deveoplopment - FfD4, kilichofanyika mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban (watatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Mhe. Innocent Shiyo (watatu kulia), Kamishna Msaidizi kutoka Wizara ya Fedha, Idara ya Fedha za Nje Bw. Patrick Pima (wapili kushoto), Afisa Dawati la Umoja wa Mataifa, Wizara ya Fedha, Idara ya Fedha za Nje, Dkt. Threza Mtenga (wapili kulia) pamoja na Maafisa wengine kutoka Wizara ya Fedha, Idara ya Fedha za Nje, walipotembelea Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia mara baada ya kumalizika kwa Kikao cha Kwanza cha Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Nne wa Kimataifa wa Ugharamiaji kwa Maendeleo Endelevu (Fouth International Conference on Financing for Deveoplopment - FfD4, kilichofanyika mjini Addis Ababa nchini humo.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha- Addis Ababa - Ethiopia).

Alisisitiza kuhusu Umoja wa Mataifa (UN) kutenga rasilimali kwa ajili ya ukusanyaji wa data, usambazaji, na matumizi ili kuhakikisha kuwa kunakuwa na ufuatiliaji mzuri wa maendeleo kuelekea Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news