DODOMA-Ujumbe wa Wataalam kutoka nchi ya Korea Kusini leo Julai 19, 2024 umekutana na wataalam wa Wizara ya Madini Tanzania na kujadiliana kuhusu fursa za Uwekezaji zilizopo katika madini mkakati aina ya Lithium yanayo patikana nchini.


Bw. Byun amesema, kupitia uwekezaji huo, zitakuwepo na fursa mbalimbali kama vile ujenzi wa miundombinu kuelekea eneo la mradi , ubadilishanaji wa teknolojia pamoja na kufungua wigo mpana wa uwekezaji na masoko wa malighafi zitokanazo na rasilimali madini.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Bw. Fredrick Mangasini amesema STAMICO ipo tayari kuingia mkataba wa makubaliano na Kampuni ya Sonokong kwa lengo kuongeza uwekezaji katika madini mkakati hususan kwa madini ya Lithium ambayo hivi sasa yanathamani kubwa duniani katika sekta nzima ya sayansi na teknolojia.
Mangasini amefafanua kuwa, STAMICO kwa kushirikiana na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) ambao wana taarifa za utafiti wa madini watatoa ushirikiano mkubwa ili kufanikisha uwekezaji huo.
Katika majadiliano hayo, Tanzania imewakilishwa na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na Tume ya Madini.

# Vision 2030: Madini ni Maisha na Utajiri