IRINGA-Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor Seff leo Julai 2,2024 ameshiriki katika ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa Barabara ya Iringa - Kilolo akiambatana na TANROADS na ujumbe wa Benki ya Dunia (WB).

Ujumbe huo wa Benki ya Dunia unatembelea Miradi ya RISE kuona kama utekelezaji wake unaendelea kulingana na Mpango wa utekelezaji uliokubalika na kuona changamoto katika utekelezaji kama zipo.

Mradi wa ujenzi wa barabara ya Iringa (Ipogolo)-Kilolo (33.61) ni wa kiwango cha lami unatekelezwa na Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) na Mkandarasi China Henan Engineering Company.
Tags
Benki ya Dunia Tanzania
Habari
Ofisi ya Rais-TAMISEMI
TANROADS Tanzania
TARURA
TARURA Tanzania
Wizara ya Ujenzi Tanzania