NA DIRAMAKINI
BENKI ya Biashara Tanzania (TCB) imezindua huduma ya Popote Akaunti inayomuwezesha mteja kufungua akaunti na kupata huduma za kibenki kidijiti pamoja na kufanya malipo mbalimbali ikiwemo kulipia tiketi za Reli ya Kisasa (SGR).
Ofisa Mkuu wa Huduma za Kidijiti na Ubunifu TCB, Jesse Jackson amebainisha hayo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo mkoani Dar es Salaam.

Jesse alisema huduma hiyo itawasaidia jamii hasa ambao wanaishi maeneo ya vijijini na walio mbali na benki.
Jesse amesema kuwa, kubuniwa kwa huduma hiyo ni mwendelezo wa dhamira thabiti ya Benki ya TCB katika kuwezesha ujumuishi wa kifedha na kutumia maendeleo ya teknolojia katika kuongeza upatikanaji wa huduma za kibenki.

Amesema kuwa benki hiyo itaendelea kubuni huduma ambazo zitasaidia kupeleka huduma za kifedha karibu na wateja nchini.

Awali Mkurugenzi wa Masoko na Ukuzaji Biashara na Mahusiano ya Umma, Deo Kwiyukwa alisema kuwa huduma hiyo inapatikana baada ya kufungua akaunti kwa gharama ya shilingi 1,000.

“Hiyo tiketi itakuwa na QR code haitaji kuiprinti ila anaweza kufanya hivyo ataionesha tu kwenye yale Magati ya kuingilia kwenye Treni ya Kisasa na kuingia moja kwa moja” amesema