Tembo Nickel imepata mafanikio ya kihistoria kwa mara ya kwanza-Waziri Mavunde

NA DIRAMAKINI

WAZIRI wa Madini,Mheshimiwa Anthony Mavunde leo Julai 23,2024 amesema, Kampuni ya Tembo Nickel ambayo Serikali ya Tanzania ni mbia,imepata mafanikio ya kihistoria kwa mara ya kwanza.
"Tembo Nickel kupitia kampuni yake mama ya Lifezone Metals imeandika historia kwa kuzalisha nikeli, shaba, na kobalt zilizosafishwa kutoka kwenye Mradi wa Kabanga Nickel ulioko Ngara, Kagera.
"Hatua hii muhimu imefikiwa wakati wa majaribio yaliyofanywa katika Maabara ya Lifezone ya kisasa ya Simulus, kwa kutumia Teknolojia yao ya ubunifu ya Hydromet.

"Mafanikio haya yanaendana kikamilifu na maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuongeza thamani ndani ya nchi.

"Uzalishaji huu ni wa mara ya kwanza katika kipindi cha karibu miongo mitano tangu ugunduzi wa madini hayo katika eneo la Kabanga.
"Kwa mafanikio haya, Tembo Nickel inaweka msingi imara kwa Kiwanda chake cha Usafishaji Metali Anuai kitakachokuwa Kahama mkoani Shinyanga ambacho kitazalisha madini ya ubora wa juu yaliyopatikana kwa kuzingatia uendelevu hapa hapa Tanzania,ambacho tayari ya Madini wameshatoa Leseni husika na hivyo kupelekea kuanza kwa hatua za awali za ujenzi wake.

"Hii ni hatua muhimu katika kuifanya nchi yetu kuwa kati ya nchi vinara duniani katika uzalishaji wa nikeli ya Daraja la 1 na madini mengine ya kimkakati.
"Tanzania iko tayari kukumbatia uwekezaji wa kuchimba madini wenye uwajibikaji na ubunifu ambao unaweka kipaumbele uongezaji wa thamani ndani ya nchi na maendeleo endelevu.

"Shirikiana nasi katika safari ya Tanzania kuelekea katika mustakabali ang’avu na wenye mafanikio zaidi katika sekta ya madini duniani,"amesisitiza Mheshimiwa Mavunde leo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news