DAR-Halmashauri ya Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam ambayo ni mshindi wa kwanza na wa jumla kwenye utoaji taarifa kwenye Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, imenunua vitendea kazi vya shilingi milioni 78 kwa ajili ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.

"Temeke tumekuwa wa kwanza na tunataka kuendelea kubaki kwenye nafasi hii, hivyo vifaa hivi ni mbinu bora ya kujipanga kuendelea kutoa taarifa bora, sahihi na kwa wakati ili tuendelee kushikilia nafasi yetu na kuhabarisha umma kazi kubwa inayofanywa na Rais wetu Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan."