TRC:Mabadiliko ya Ratiba na Ongezeko la Safari za Treni za SGR kuanzia Julai 5,2024

DAR-Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetangaza kuanza kwa safari ya treni ya haraka (express train) ya reli ya kiwango cha kimataifa - SGR ambayo itakuwa ikifanya safari kati ya Dar es Salaam na Morogoro bila kusimama vituo vya kati.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Julai Mosi,2024 na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano -TRC, Jamila Mbarouk.

Amesema, ujio wa treni hiyo umekuja na mabadiliko ya ratiba za treni kati ya Dar es Salaam na Morogoro kuanzia Julai 5, 2024.

Mbarouk amesema, treni ya haraka itakuwa ikiondoka Dar es Salaam saa 12:00 asubuhi na saa 1:10 usiku, na itaondoka Morogoro saa 12:20 asubuhi na saa 1:30 usiku.

Treni ya kawaida itakuwa ikiondoka Dar es Salaam saa 3:30 asubuhi na saa 10:00 jioni na itaondoka Morogoro saa 3:50 asubuhi na saa 10:20 jioni.

Amewashauri abiria kukata tiketi kupitia njia ya mtandao au madirisha ya tiketi yaliyopo ndani ya vituo vya treni saa mbili kabla ya muda wa safari ili kuepuka msongamano.

Pia,amesema shirika litaendelea kuongeza idadi ya safari kulingana na ongezeko la idadi ya abiria ili kutoa huduma bora na za uhakika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news