Tuchangie Mfuko wa Bima ya Afya kwa Wote-Dkt.Jingu

DAR-Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu amewaomba wadau wa maendeleo ndani ya Sekta ya Afya kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali hususani kipindi hiki cha kuelekea kwenye utekelezaji wa mpango wa Bima ya Afya kwa wote nchini.
Dkt. Jingu ametoa wito huo leo Julai Mosi, 2024 jiji Dar Es Salaam wakati wa kikao kazi cha kuridhia mpango kazi na matumizi ya fedha zinazotolewa kupitia mfuko wa pamoja wa afya zikiwemo Balozi, na Benki ya Dunia kwa mwaka wa fedha 2024/25.
Dkt. Jingu amesema,Sheria ya Bima ya Afya kwa wote iliyosainiwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan inalengo la lakuona kila Mtanzania anapata huduma bora za Afya muda wote hasa kwa makundi maalum wakiwemo mama wajawazito, watoto chini ya miaka mitano na wananchi wasio na uwezo.
“Wadau wa sekta ya Afya wamekuwa wakiunga mkono juhudi za serikali kwa kuchangia kupitia mfuko wa afya ya jamii(CHF) na kuimarisha huduma za afya nchini, hivyo niwaombe kuendelea kuunga mkono utekelezaji wa mpango wa Bima ya Afya kwa wote unatakao kuwa mkombozi kwa wananchi wasio na uwezo,”Dkt. Jingu amesema.

Aidha, Dkt. Jingu amewashukuru wadau kwa kuendelea kuchangia bajeti ya wizara ya afya ambayo imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka kwa kipindi cha miaka mitatu iiyopita.
Awali akimkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu, Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu alisema Serikali kupitia Wizara ya Afya imeendelea kuimarisha ubora wa huduma za afya na kusogeza karibu na Wananchi hadi katika ngazi za msingi.

“Kwa sasa kila mtanzania anapata huduma bora za afya kwani tumepeleka madaktari bingwa na ubingwa bobezi kwenye hospital za wilaya ambapo mbali ya kutoa huduma kwa wananchi pia wamewajengea uwezo na ujuzi kwa watumishi wa afya katika hospitali hizo,” amesema Prof. Nagu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news