Tuendelee kuiunga mkono Serikali inayoongozwa na Rais Dkt.Samia-Mheshimiwa Ridhiwani

PWANI-Mbunge wa Jimbo la Chalinze na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete amewakumbusha wananchi jimboni humo kuendelea kuiunga mkono Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Amesema, Serikali imeendelea kufanya mambo makubwa ikiwemo utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kama ilivyo kwa Kata ya Kiwangwa jimboni humo.
Mheshimiwa Ridhiwani ameyasema hayo hivi karibuni baada ya kufanya mkutano huko Kiwangwa na kuwapongeza wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika mfumo wa Kidijitali.
Hata hivyo, Mhe. Ridhiwani alizunguka katika matawi mbalimbali na kuzungumza na wanachama wapya wa CCM na kuwasisitiza wananchi kuhusu uandikishaji wa kadi za kupiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa,vijiji na vitongoji pamoja na uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news