Tunataka kuona TAFORI iliyoboreshwa-Waziri Kairuki

NA HAPPINESS SHAYO

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) ametoa rai kwa Watumishi wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) kutimiza wajibu wao kuhakikisha Taasisi hiyo inaboreka na hatimaye kuchangia katika mapato ya Taifa.
Ameyasema hayo leo katika ziara yake ya kikazi alipotembelea taasisi hiyo kwa lengo la kuangalia utendaji kazi, kusikiliza changamoto za watumishi na kuzipatia ufumbuzi.
Amesema, katika kufikia malengo ya Taasisi ni lazima wakawa wabunifu katika utekelezaji wa majukumu yao huku Serikali ikifanyia kazi changamoto za bajeti, vitendea kazi na upungufu wa Watumishi wote zinazowakabili.

"Fuatilieni fursa za mafunzo ili kukuza utendaji kazi wenu na mjitoe kufanya kazi kwa bidii na msikate tamaa,"amesisitiza.
Aidha,amewataka watumishi hao kujiwekea mipango mbadala ya kuiongezea Taasisi hiyo mapato kwa kuandika maandiko mbalimbali ya kuomba fedha katika Taasisi zinazotoa fedha hizo akitolea mfano wa Earth Fund na nyinginezo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news