Tundu Lissu asema mwakani atawania urais Tanzania

DAR-Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tanzania Bara, Mheshimiwa Tundu Lissu amesema, nia ya kugombea urais mwaka 2025 iko pale pale.
Lissu ameyasema hayo leo Julai 26,2024 alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam akitokea nchini Ubelgiji.

"Nilipokuwa ninamkabili Magufuli (Hayati Dkt.Jonh Pombe Joseph Magufuli) nilikuwa na miaka 52,mwaka ujao nitakuwa na miaka 57. Kwa hiyo haiwezi nikawa nina nguvu zile zile za miaka 52, lakini nguvu ya hoja.

...nguvu ya hoja na msimamo wa kisiasa na uaminifu kwa Watanzania bado uko pale pale, kama tuliweza kumkabili Magufuli nia iko pale pale, nitaitikia wito wa Watanzania na nitaitikia wito wa chama changu,"amesisitiza Mheshimiwa Lissu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news