Tuzo ya ushindi Sabasaba yafikishwa kwa Dkt.Yonazi, atoa wito

DODOMA-Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amesema Tuzo ya Ushindi wa Kwanza kwa Ofisi yake kwa kundi la watoa huduma bora na banda bora ngazi ya za wizara zilizoshiriki katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es salaam iwe nguzo ya kutoa huduma bora na kwa upana zaidi kwa wananchi.
Ameyasema hayo mapema leo tarehe 17 Julai, 2024 baada ya kupokea tuzo hiyo Ofisini kwake Jijini Dodoma ambapo Dkt. Yonazi alitoa shukrani kwa viongozi wa Ofisi hiyo na Taasisi zake kwa maandalizi mazuri na kuongeza kusema kuwa, tuzo hiyo pia itawezesha Ofisi kufikia malengo ya Serikali na Maono ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ya kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuleta tija kwa Taifa.
“Ninaamini mwakani tunaweza kufanya vizuri zaidi kwa kuchukua ushindi wa jumla na siyo katika hutoaji huduma bora na banda bora, hivyo hii iwe kama chachu ya kuamsha morali ya kazi kwa watumishi wote wa Ofisi ya Waziri Mkuu.”

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Bw. Anderson Mutatembwa alitoa pongezi kwa timu nzima iliyoshikiri katika maandalizi hayo na kusema hii ni dalili nzuri inayoonesha utekelezaji wa maagizo na miongozo yanayotolewa na viongozi wa ngazi za juu.
Awali, akiongea wakati wa kaukabidhi Tuzo Hiyo Mwenyekiti wa kamati hiyo ya Maandalizi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Uwekezaji na Uwezashaji wananchi kiuchumi, Kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Bw. Condrad Millinga alisema kupitia maonesho hayo wananchi waliofika katika banda hilo walipata nafasi ya kufahamu majukumu yanayotekelezwa na ofisi pamoja na taasisi zake.
“Wanachi walipata elimu kuhusu namna tunavyotekeleza majukumu ya Ofisi pamoja na kuwahudumia kwa ubora, hii ilichangia kuongeza tija ya uwepo wa banda la Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zake katika maonesho hayo,”alieleza Millinga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news