LINDI-Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amesema ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa Bandari ya Uvuvi ya Kilwa Masoko ambao mpaka sasa umefikia asilimia 63 na unatarajiwa kukamilika mwezi Februari, 2025.
Waziri Ulega amesema hayo leo Julai 30,2024 wakati akikagua maendelea ya ujenzi wa mradi huo unaofanyika wilayani Kilwa mkoani Lindi.
Amesema, bandari hiyo ya uvuvi inayojengwa kwa fedha za ndani ni mradi wa kielelezo unaotekelezwa chini ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
“Mradi huu tuutazame kama mboni ya jicho letu ili uwe endelevu kwa maana ukikamilika utainua uchumi wa Kilwa, ukanda wa Kusini na Taifa kwa ujumla.