Umeme utaongeza uzalishaji wa madini mkoani Katavi-Waziri Mavunde

KATAVI-Waziri wa Madini,Mheshimiwa Anthony Mavunde amewaeleza wachimbaji wa Mkoa wa Katavi kwamba utekelezaji wa mradi wa kuingiza Katavi kwenye Gridi ya Taifa itasaidia upataikanaji wa uhakika wa umeme na hivyo kupelekea kuongezeka kwa uzalishaji wa madini mkoani humo.
Waziri Mavunde alimeyasema hayo Julai 14, 2024 Mpanda mkoani Katavi wakati wa kikao cha pamoja kati yake na uwakilishi wa wachimbaji mkoani Katavi ikiwa ni muendelezo wa ziara ya kikazi ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoani humo.
“Tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji mkubwa wa mradi wa umeme ambao umelenga kuuingiza mkoa wa Katavi kwenye gridi ya Taifa na hivyo kusaidia upatikanaji wa umeme wa uhakika,"amesema Mhe.Mavunde.

Mhe.Mavunde aliongeza kuwa, baada ya Katavi kuingia kwenye gridi ya Taifa,uzalishaji wa madini utaongezeka maradufu kuliko hivi sasa na hivyo kupelekea kuongezeka kwa mapato yatokanayo na sekta ya madini.
Kuhusu suala la tozo zinazongezeka mara kwa mara kupitia Mamlaka za Halmashauri za Wilaya na Manispaa, tutakutana na Waziri wa TAMISEMI ili tulizungumze hili kwa pamoja na kulipatia muafaka jambo hili.”

Akitoa salamu za wachimbaji, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wachimba Madini Mkoa wa Katavi (KATAREMA), William Mbogo ameishukuru Serikali na Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa utashi wake wa kukuza sekta ya madini nchini kwa kuiongezea Bajeti Wizara ya Madini kufikia shilingi bilioni 231 ili kusaidia kufanya utafiti wa kina nchi nzima kwa lengo la kuwawezesha wachimbaji wadogo kuchimba bila kubahatisha.
Aidha, Mbogo amemuomba Waziri wa Madini kushughulikia matatizo yaliyowasilishwa ikiwemo suala la upatikanaji wa nishati ya umeme wa uhakika na tozo zilizokithiri zilizotambulishwa na Halmashauri za Wilaya na Manispaa ambazo zinakwenda kuathiri suala la uchimbaji kwa kiasi kikubwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news