NJOMBE-Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) wameagizwa kuhakikisha Chuo cha VETA cha Mkoa wa Njombe kinapelekewa vifaa vya kufundishia na kujifunzia ili kianze kutoa mafunzo kwa wakazi wa mkoa huo.
Agizo hilo limetolewa Julai 19, 2024 mkoani humo na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Franklin Rwezamula alipofika chuoni hapo kukagua ujenzi wa miundombinu hiyo ambapo alisema ameridhishwa na ukamilishaji wa miundombinu majengo hayo.
Dkt. Rwezamula ameongeza kuwa majengo yote muhimu kukiwezesha chuo kuanza kutoa mafunzo kwa wananchi wa Njombe yamekamilika na kwamba si sahihi yakakaa muda mrefu bila kutumika.

Chuo cha VETA cha Mkoa wa Njombe kimejengwa katika wilaya ya Ludewa karibu sana na Mchuchuma na Liganga ambapo panapatikana makaa ya mawe pamoja na chuma.