VIDEO:Huduma za Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali zawapa faraja wananchi Maonesho ya Sabasaba

DAR- Banda la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba 2024) limeendelea kuwa kivutio kwa wananchi wengi ambao, kadri wanavyofika katika banda hilo licha ya kupokelewa na wataalamu mbalimbali kwa ukarimu, pia wamekuwa wakipatiwa huduma kwa haraka ikiwemo elimu.
Ofisi hiyo ni miongoni mwa taasisi za umma ambazo zinashiriki maonesho hayo ambayo yanafanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere vilivyopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Maonesho hayo yalifunguliwa Juni 28,mwaka huu, yakafunguliwa rasmi Julai 3 na Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi na yanatarajiwa kufungwa rasmi Julai 13 mwaka huu.
Wananchi wakielezea furaha yao baada ya kuhudumiwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Maonesho ya SabaSaba.Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali tupo SabaSaba ndani ya Banda la Mahakama.

Karibu sana Tukuhudumie.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news