DODOMA-Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imezishukuru taasisi mbalimbali ikiwemo Wizara ya Katiba na Sheria, Chama cha Mawakili wa Serikali, Wizara ya Ardhi, Tume ya Utumishi wa Walimu, Uhamiaji na taasisi zingine za Serikali kwa kujitokeza na kuwahudumia wananchi wakati wa uendeshaji wa Kliniki ya Sheria.
Ni iliyolenga kutoa msaada wa kisheria bure kwa wananchi na kufanya utatuzi wa migogoro mbalimbali kuanzia Juni 26 hadi Julai 3, 2024 katika Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
Akizungumza mara baada ya kuahirisha kliniki hiyo ya siku nane ambayo lilizinduliwa rasmi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi, Kaimu Mkurugenzi wa Divisheni ya Uratibu na Huduma za Ushauri, Bi. Neema Ringo amesema Kliniki hiii ililenga kupata suluhu ya matatizo ya kisheria yanayowakabili wananchi, kuyatatua na kutafuta utaratibu wa kutoa mrejesho kwao ambapo imeonesha kuwa na ufanisi mkubwa.
Aidha, alisema katika kliniki zitakazofuata hapo baadae , wananchi watafuatwa katika maeneo yao ili kuwafikia wanachi wengi zaidi na kupunguza adha kwa wananchi kuifuata huduma ilipo. Tazama video chini;