MWANZA-Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mheshimiwa Said Mohamed Mtanda amewataka Askari wa Jeshi la Polisi wakiwemo watumishi wa umma kuzingatia weledi na kutojihusisha na vitendo vya rushwa wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kila siku.
Mheshimiwa Mtanda ameyasema hayo hivi karibuni jijini Mwanza kwenye sherehe za kuwatunuku Hati ya Sifa na Pongezi askari tisa waliofanya vizuri kazini, ambapo kwenye hafla hiyo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) walikuwa mstari wa mbele kutoa elimu.
"Hapa ninawataka Askari wa Jeshi la Polisi kuzingatia weledi na kutojihusisha na vitendo vya rushwa. Biblia imeandika rushwa hupofusha hao waonao,ukishakula rushwa hauwezi kuona gari yenye matairi mabovu.
Rejea katika Biblia Takatifu,
Kutoka 23:8 “Nawe usipokee rushwa; kwani hiyo rushwa huwapofusha macho hao waonao, na kuyapotoa maneno ya wenye haki”.
Kumbukumbu 16:19 “Usipotoe maamuzi; wala usipendelee uso wa mtu; WALA USITWAE RUSHWA; KWA KUWA RUSHWA HUPOFUSHA MACHO YA WENYE AKILI, NA KUGEUZA DAAWA YA WENYE HAKI”.
"Kwa hiyo utaacha gari iende halafu inabasti matairi,watu wanakufa kwa uzembe na kwa rushwa,watu wengi wanapoteza maisha yao. Kwa hiyo nitoe rai kwa Jeshi la Polisi na watumishi wote wa Serikali ndani ya Mkoa wa Mwanza kuacha kujihusisha na vitendo vya rushwa.
"Na mimi Mkuu wa Mkoa nitakuwa mfano na mstari wa mbele, kuhakikisha kwamba mimi mwenyewe ninakuwa taswira bora kwa hiki ninachosema, viongozi tunawajibika yale tunayoyasema na ndiyo tunayasimamia na kuyatekeleza;
Tags
Habari
Rushwa ni Adui wa Haki
Rushwa ni Upofu
Said Mohamed Mtanda
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)
TAKUKURU Tanzania