VIDEOS:Dkt.Mwasaga aweka wazi mikakati ya Serikali kuwa kitovu cha Uchumi wa Kidigitali

DAR-Julai 16, 2024 Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA nchini,Dkt.Nkundwe Mwasaga alifanya mahojiano mubashara na runinga ya Channel Ten ambapo aliangazia kwa kina mafanikio ya TEHAMA hapa nchini.
Je? Kuna mikakati ya kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha Uchumi wa Kidigitali?

Dkt.Nkundwe Mwasaga anasema kuwa, mikakati ipo mingi sana, "kama umemwangalia Mheshimiwa Rais kwa mara kadhaa ameweza kutuambia kwamba anataka kuona Watanzania wanakuwa na namba za Kidigitali na vile vile kuona mifumo inazungumza.

"Sasa hilo jambo ni jambo kubwa sana. Kiukweli kimkakati kwa sababu nchi nyingi sasa hivi duniani zimeondoka katika ile hali ya kutengeneza mifumo mbalimbali kuhakikisha kwamba Uchumi unaondoka katika Analojia kuja Kidigitali.

"Sasa wameenda katika kuhakikisha watu wanapata huduma vizuri, watu wanaweza kutumia TEHAMA kufanya shughuli zao, kuweza kupata mikopo kuhakikisha kwamba mifumo mbalimbali wanayoitumia wanaitumia kwa namna ambayo ni salama, taarifa zao zinatunzwa vizuri.

"Na hayo yote yanaweza kufanyika pale ambapo utahakikisha kwanza mifumo inaweza kuongea yenyewe. Halafu uwe na namba moja, ambayo hiyo namba ndiyo tutakayoitumia kuangalia au uweze kupata huduma mbalimbali zinazotolewa na Serikali.
"Sasa ile katika namna kubwa kiuchumi itaweza kutusaidia kupata faida kubwa ya sekta ambayo siyo rasmi ambayo kwetu hapa ni kubwa kuitoa katika isiwe rasmi kuwa rasmi.

"Na nchi ambazo zimefanya hicho tumeona kabisa mapato wanayopata kwa kukusanya kodi yanakuwa yanaongezeka. Tumeona imetokea kwa India na nchi nyingi ambazo zimefanya hivyo.

"Kwa hiyo mkakati wetu sasa hivi tunaenda kwenye digitalization kuhakikisha hiyo process ya Kidigitali inaenda haraka, watu wanapata namba za Kidigitali, mifumo yote inaanza kuzungumza vizuri ili tuweze kufanya mapinduzi sasa ya Kidigitali unayoyasikia."

Mafanikio makubwa katika Sekta ya TEHAMA 
Maendeleo ya teknolojia na usalama wa ajira kwa vijana 
Mfahamu Roboti Eunice 
Kuhusu e-Government

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news