VIDEOS:Roboti hawezi kuchukua kazi ya mtu-Dkt.Mwasaga

DAR-Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA nchini,Dkt.Nkundwe Mwasaga amewatoa hofu wale ambao wanadhani kuwa ujio wa roboti unaweza kusababisha watu kukosa ajira.
Dkt.Mwasaga ameyasema hayo leo Julai 19,2024 wakati akifanya mahojiano katika Kipindi cha Kumepambazuka kinachorushwa na Redio One iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

"Kazi kwa kawaida ina majukumu...halafu ina vitu ambavyo unatakiwa uvifanye, ina ile ambayo tunaita wajibu na majukumu uliyokuwa nayo.

"Wajibu ndiyo vile vinakusaidia kupandishwa vyeo au kama ukikosea unashushwa huo ni wajibu. Roboti hana hicho kitu, hawajibiki hicho cha kwanza.
"Roboti anafanya task fulani tu, hana uwezo wa kufanya kazi nzima. Kwa mfano nyie mmenialika hapa katika kipindi cha leo kuna maandalizi ambayo mmefanya kweli si kweli?...

"Sasa ukisema tu mwandishi wa habari kazi yake ni kutangaza, unaacha kuna kazi zingine nyingi anazifanya mpaka kufika wa kutangaza hizo zote ndiyo zina ku-define wewe kazi yako.

"Kwa hiyo roboti anaweza kufanya task moja. Anaweza akafagia,lakini mfagizi hafagii hewani anafagia ofisini kuna namna anaongea na binadamu aliyepo ile yote ile ndiyo kazi. Ile kufagia ni task moja tu.
"Kwa hiyo roboti mpaka sasa hivi hawezi kuchukua kazi ya mtu kwa sababu kazi moja inakuwa na tasks nyingi ila anaweza akafanya task moja vizuri,"amesisitiza Dkt.Nkundwe Mwasaga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news