Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) chini ya Wizara ya Kilimo imeanzishwa kwa Sheria ya Mbolea Na. 9 ya mwaka 2009.
Aidha,mwaka huu ni miongoni mwa taasisi za umma ambazo zinashiriki katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba vilivyopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.
MAJUKUMU YA TFRA
1. Kusimamia na kudhibiti ubora wa mbolea nchini.
- Kusajili mbolea.
- Kufanya ukaguzi wa ubora wa mbolea katika mnyororo wa tharnani.
2. Kudhibiti utengenezaji, uingizaji na biashara ya mbolea nchini.
- Kusajili, kutoa leseni, na kutunza kumbukumbu za watengenezaji na wauzaji wote wa mbolea.
- Kutoa vibali vya watengenezaji, waagizaji, wasambazaji wa mbolea nchini na wauzaji wa mbolea nje ya nchi.
- Kusimamia bei za mbolea nchini.
- Kuunganisha wauzaji na wanunuzi wa mbolea nchini ili kuhakikisha kwamba mbolea inayotosheleza inapatikana kwa wakati.
3. Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Serikali na taasisi zingine juu ya masuala yanayohusu sera za usimamizi na udhibiti wa ubora na biashara ya mbolea.
4. Kushirikiana na asasi za ndani na nje ya nchi zinazoshughulikia mbolea katika kuhakikisha mbolea inamfikia mkulima katika ubora unaokubalika na bei nafuu.
5. Kushirikiana na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kuelimisha Umma juu ya matumizi sahihi ya mbolea.
Tags
Habari
Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania
Maonesho ya 48 ya Biashara ya Sabasaba
TFRA Tanzania