Viwanja 4,150 vyamilikishwa katika mitaa 270 Dar

NA MUNIR SHEMWETA

JUMLA ya viwanja 4,150 vimemilikishwa katika mitaa 270 ya mkoa wa Dar es salaam kupitia programu ya ukwamuaji urasimishaji pamoja na klinik ya ardhi katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Machi 2024.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akizungumza wakati wa mkutano wa kupokea taarifa ya utekelezaji zoezi la ukwamuaji kazi ya urasimishaji mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika kwenye Jimbo la Ukonga katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam tarehe 1 Julai 2024.

Aidha, programu hiyo imewezesha viwanja 55,034 kupangwa na vingine 6,824 kupimwa sambamba na elimu kutolewa kwa kamati za urasimishaji za mitaa 46 ambapo jumla ya viwanja 2,727 vinavyotakiwa kumilikishwa vimeibuliwa.
Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Njombe, Mhe. Neema Mgaya akimkabidhi mkazi wa Ukonga hati milki ya ardhi kwenye mkutano wa kupokea taarifa ya utekelezaji zoezi la ukwamuaji kazi ya urasimishaji mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika Ukonga manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam Julai 1, 2024.

Hayo yamebainishwa leo Julai 1, 2024 mkoani Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Geophrey Pinda wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii ilipopokea taarifa ya utekelezaji zoezi la ukwamuaji urasimishaji katika jimbo la Ukonga Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mhe. Pinda, miradi ya urasimishaji katika halmashauri za mkoa wa Dar es Salaam ilianza kutekelezwa mwaka 2013 ambapo hadi kufikia mwezi Desemba 2023 jumla ya viwanja 565,690 vilikuwa vimepangwa ambapo viwanja 132,811 vilipimwa na viwanja 42,513 vilimilikishwa.Sehemu ya washiriki wa mkutano wa kupokea taarifa ya utekelezaji zoezi la ukwamuaji kazi ya urasimishaji katika mkoa wa Dar es Salaam wakiwa katika mkutano uliofanyika Ukonga jijini Dar es Salaam Julai 1, 2024.

"Takwimu hizi zinaonesha kuwa, utekelezaji wa programu ya urasimishaji wa makazi yasiyopangwa ulikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kasi ndogo ya upimaji na umilikishaji wa viwanja vilivyopangwa," amesema Mhe. Pinda.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Ardhi Maliasili na Utalii Mhe. Timotheo Mzava akimkabidhi mkazi wa ukonga hati milki ya ardhi wakati wa mkutano wa kupokea taarifa ya utekelezaji zoezi la ukwamuaji kazi ya urasimishaji katika mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika jimbo la Ukonga tarehe 1 Julai 2024.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii, Mhe. Timotheo Mzava ameishukuru Serikali kwa kuwezesha ukwamuaji urasimishaji maeneo ya makazi holela kupitia Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki (LTIP) hasa ikizingatiwa zoezi hilo halikwenda vizuri siku za nyuma.

"Wenzetu wa wizara ya Ardhi wamefanya vizuri sana katika zoezi la ukwamuaji urasimishaji lakini niwatake wananchi kutoa ushirikiano wakati wa utekekezaji zoezi hilo na kwa upande wa wizara waongeze kasi ya utekelezaji zoezi ili wananchi waweze kumilikishwa kwa hati,"amesema Mhe. Mzava.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ardhi Maliasili na Utalii wakiwa kwenye mkutano wa kupokea taarifa ya utekelezaji zoezi la ukwamuaji kazi ya urasimishaji katika mkoa wa Dar es Salaam wakiwa katika mkutano uliofanyika katika jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam tarehe 1 Julai 2024.

Katika ziara yake, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii ilipokea taarifa ya utekelezaji zoezi la ukwamuaji kazi za urasimishaji katika mkoa wa Dar es Salaam, kuongea na kamati za urasimishaji za manispaa ya ilala pamoja na kugawa hati milki za ardhi kwa wananchi.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ardhi Maliasili na Utalii wakiwa katika picha ya pamoja na wananchi wa jimbo la Ukonga waliokabidhiwa hati milki za ardhi kwenye mkutano wa kupokea taarifa ya utekelezaji zoezi la ukwamuaji kazi ya urasimishaji katika mkoa wa Dar es Salaam tarehe 1 Julai 2024. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI).

Aidha, katika siku yake ya kwanza ya ziara yake jijini Dar es Salaam, kamati hiyo ilikagua miradi inayotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news