Waganga Wakuu toeni mafunzo ya kuepusha ajali za bodaboda-Waziri Mchengerwa

NA JAMES MWANAMYOTO
OR-TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuwa na utaratibu wa kutoa mafunzo kwa madereva wa bodaboda kupunguza ajali zinazoepukika.
Mhe. Mchengerwa ametoa maelekezo hayo akiwa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salam, wakati akizindua sare maalum (uniform) na mfumo wa kidijitali (kanzidata) wa madereva Bodaboda na Bajaji wa jiji la Dar es Salaam.

“Tumesikia hapa takwimu za ajali na vifo vinazotokana na ajali za bodaboda nchini, hivyo Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya wekeni utaratibu wa kutoa mafunzo ya usalama wa afya za maafisa usafirishaji hawa wa bodaboda ili waepukane na ajali,” Mhe. Mchengerwa amesisitiza.
Mhe. Mchengerwa amewataka Wakuuu wa Mikoa kuhakikisha wanasimamia utekelezaji wa agizo lake la mafunzo, ili yaanze kutolewa mapema iwezekanavyo kwa lengo la kuepusha ajali na kulinda uhai wa madereva bodaboda na wasafiri wanaotumia vyombo hivyo ambao wengi wao ni nguvu kazi ya taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news