Wakorea wavutiwa na ufanisi wa miradi ya NHC nchini

NA GODFREY NNKO

UJUMBE kutoka Jamhuri ya Korea Kusini ukiongozwa na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Fedha ya Korea kwa ajili ya Ujenzi (K-Finco), Dkt. Lee Eun Jae umeonesha kuguswa na namna ambavyo Shirika la Taifa la Nyumba nchini (NHC) linavyotekeleza miradi yake kwa ubora na kwa kiwango cha Kimataifa.
Hayo yamejiri leo Julai 27,2024 baada ya ujumbe huo ambao pia umeongozwa na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Jamhuri ya Korea Kusini, Mheshimiwa Togolani Mavura kuitembelea baadhi ya miradi ya shirika hilo jijini Dar es Salaam.

Ujumbe huo upo nchini kufuatia wito wa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kuchangamkia fursa za uwekezaji katika sekta ya nyumba na maeneo mengine.
Awali, Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), William Genya amewaonesha wajumbe hao eneo la Upanga Mashariki jijini Dar es Salaam ambalo linatarajiwa kuendelezwa na shirika hilo kwa kushirikiana na wadau.

Vile vile ujumbe huo umetembelea mradi wa NHC, Kawe Seven Eleven (7/11) ambapo wameshuhudia utekelezaji ukifanyika kwa kasi kubwa.

Kazi waliyoikuta imefanyika ni kubwa, ambapo mradi huo kupitia majengo marefu ya kisasa yameanza kubadili mandhari ya Kawe na kulifanya eneo ulipo mradi kuwa la kuvutia zaidi.
Muonekano wa Upanga Mashariki.

Kilichowavutia zaidi wajumbe hao ni kushuhudia ujenzi huo ambao unatekelezwa na kampuni ya ujenzi ya Esteem Construction, wazawa wanafanya kazi kwa bidii.

7/11 huu ni mradi wa makazi ambao pia unajumuisha maduka kwa ajili ya kupangisha watu mbalimbali.

Katika nyumba za makazi zimegawanyika katika makundi mbalimbali ikiwemo ya vyumba viwili, vitatu na vinne.

Aidha, nyumba za vyumba vitatu zimegawanyika katika makundi mawili kwa maana ya vyumba vya kawaida na kundi lingine ni la ghorofa ndani ya ghorofa.

Mkurugenzi wa Ubunifu wa NHC, Emmanuel Moshi ameueleza ujumbe huo kuwa, mradi wa 7/11 ni miongoni mwa miradi ya kisasa zaidi ambayo inatekelezwa na shirika hilo.
Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), William Genya akiwaonesha wajumbe hao eneo la Upanga Mashariki.

Mradi huu ulikuwa umekwama kwa miaka kadhaa, lakini baada ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuingia madarakani aliruhusu shirika kuchukua mkopo ili kuukwamua, matokeo yake tangu mradi uanze mapema mwaka huu mambo yamekuwa mazuri zaidi na kila mtu anatamani kuwa na nyumba ndani ya mradi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news