Wanafunzi na wakufunzi kutoka chuo cha kijeshi Zimbabwe watembelea Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt.Salim Ahmed Salim (CFR)

DAR-Ujumbe wa Wanafunzi na Wakufunzi 31 kutoka Chuo cha Kijeshi cha Ukamanda na Unadhimu cha Zimbabwe wakiongozwa na Naibu Kamanda, GC Joyce Maeresera leo Jumatatu tarehe 29 Julai 2024 wametembelea Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim (CFR).
Akizungumza wakati wa ziara hii Naibu Kamanda GC Joyce Maeresera amesema, lengo la ziara hii ni kujifunza masuala ya kiulinzi, kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Kituo Dkt. Felix Wandwe, ndc pamoja na mambo mengine yaliyofanyika wakati wa ziara hii, ameushukuru Uongozi wa Ujumbe huu kutoka Zimbabwe kwa ziara yao ya kukitembelea Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim (CFR).
Dkt. Felix Wandwe, ndc amesema Kituo kinatoa mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu katika masuala ya Diplomasia, Uhusiano wa Kimataifa, Stadi za Stratejia, Usuluhishi wa migogoro na Ujenzi wa Amani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news