Wanne hatiani kwa ubadhirifu fedha za urasimishaji makazi Kipunguni A Ilala

DAR-Mahakama ya Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam imewatia hatiani waliokuwa viongozi wa Kamati ya Urasimishaji Makazi eneo la Kipunguni "A" katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa ubadhirifu wa fedha za urasimishaji makazi shilingi milioni 10.
Ni kupitia kesi ya Jinai namba CC.386 /2024 ambayo hukumu imetolewa Julai 5,2024 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Gloria Nkwera, katika shauri lililoendeshwa na Mawakili Waandamizi wa Serikali, Veronica Chimwanda na Fatuma Waziri.

Katika kesi hiyo, Ahmed Waziri Msika na wenzake Humphrey Mwakalinga, Mohammed Magwila  na Kisura Byakuzana walitiwa hatiani kwa kosa la ubadhirifu na Ufujaji kinyume na kifungu cha 28(2) Cha PCCA [Sura ya 329 marejeo ya mwaka 2022].

Ilidaiwa kwamba,wanne hao wakiwa viongozi wa Kamati ya Urasimishaji Makazi eneo la Kipunguni "A" katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam walifuja shilingi milioni 10 zilizokuwa zimekusanywa na wananchi kwa ajili ya urasimishaji wa makazi yao.

Washtakiwa walifanya makubaliano (plea bargaining) na wamelipa fedha hizo serikalini na kuamriwa kutokufanya makosa yanayofanana na waliyoshtakiwa nayo kwa kipindi cha miaka mitatu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news