DAR-Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban ameongoza ujumbe wa Serikali katika mkutano wa wataalam wa Kamati ya Mawaziri wa Fedha na Uwekezaji na Jopo la Uchumi Jumla wa nchi zilizopo katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ulionza tarehe 29 hadi 31 Julai 2024.
Mikutano hii itajadili masuala mbalimbali ikiwemo uanzishwaji wa mfuko wa kifedha wa kanda, kujadili taarifa ya tathmini ya hali ya uchumi kwa nchi wanachama ikiwemo Tanzania, taarifa ya mgombea atakayeiwakilisha SADC katika uchaguzi wa nafasi ya Rais wa AfDB, kupokea na kujadii taarifa mbalimbali za kamati ndogo zilicho chini ya SADC.


Mikutano hii itafuatiwa na mkutano wa Mawaziri wa Fedha na Uwekezaji na Magavana wa Benki Kuu za nchi wanachama wa SADC tarehe 6 na7 Agosti 2024.