Waziri Bashe asema Rais Dkt.Samia hataki utani Kilimo cha Umwagiliaji

KIGOMA-Waziri wa Kilimo,Hussein Bashe amewahakikishia Watanzania kuwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuleta mapinduzi sekta ya Umwagiliaji, hivyo miradi yote aliyoahidi itatekelezwa.
Waziri Bashe amesisitiza utekelezaji wa miradi hiyo unaofanywa na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji si hadithi bali umelenga kuinua sekta ya Kilimo cha Umwagiliaji na kuchochea ukuaji wa uchumi nchini.

Ameitakata Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kujipanga kuhakikisha wanatekeleza miradi hiyo na wananchi wapuuze wanaowalaghai kuuza mashamba.
Waziri Bashe amesema hayo Wakati akizungumza na wadau wa umwagiliaji katika eneo la mradi wa Luiche, ambapo amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha utekelezaji wa mradi huo.

“Leo tumefanya uzinduzi wa Mradi mkubwa wa Umwagiliaji katika Bonde la Luiche Wilayani Kigoma katika Mkoa wa Kigoma.Miradi hiyo yenye thamani ya zaidi ya bilioni 60 itakwenda kunufaisha zaidi ya wakulima 9312 kupitia kilimo cha Umwagiliaji.
Ameongeza kuwa, wizara inamshukuru Rais Dkt.Samia kwani anafanya kwa vitendo na hataki utani katika kilimo cha umwagiliaji.

“Tunamshukuru sana sana Rais kwa kutoa bilioni 60 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa Luiche . Msiuze aridhi yenu ambayo serikali inawekeza fedha zaidi ya bilioni 60 kwa ajili yenu.

"Mkoa wa Kigoma ni Mlango wa uzalishaji na mlango wa kuhudumia nchi jirani.Serikali inakwenda kujenga Jengo la ghorofa tatu ambalo litakuwa kitovu cha umwagiliaji katika mkoa wa kigoma na Ghala lenye uwezo wa kuhifadhi zaidi ya tanı 4000, Pamoja na mtambo wa kuchakata mpunga,"alisema Waziri Bashe.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Raymond Mndolwa amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha utekelezaji wa mradi wa Bonde la Luiche, ambao umekuwa ukizungumzwa toka nchi ilipopata Uhuru na kwamba uwekezaji huo mkubwa uliyofanywa na serikali unakwenda kuleta mapinduzi makubwa kiuchumi kwa wananchi wa Kigoma.

Mndolwa pia ametumia fursa hiyo kupokea maagizo ya Waziri wa Kilimo.“Mradi huu ni mkubwa na utazingatia uwekaji wa miundo mbinu muhimu kama bara bara na itazingatia Kulinda vyanzo vya maji na mazingira,”alisema Mndolwa.
Mndolwa pia aliongeza kuwa Tume imepokea maelekezo ya Serikali kuwa mradi ujumuishe ujenzi wa Ghala,nyumba ya watumishi Pamoja na Ofisi ya Umwagiliaji.

Wakati akiwasilisha Taarifa ya Umwagiliaji kwa Mkoa wa Kigoma, Mhandisi Umwagiliaji Mkoa wa Kigoma, Mhandisi Katuta Mustang, amesema Mkoa wa Kigoma Una eneo linalo faa kwa umwagiliaji lenye ukubwa wa Hekta 147,000 na kwamba Mkoa wa Kigoma una jumla ya skimu za umwagiliaji 59 na ni skimu 6 pekee ndizo zilizoendelezwa.

“Mradi wa Ruiche unajumuisha ujenzi wa Skimu kwa gharama ya shilingi Bilioni 40 na ujenzi wa Bwawa lenye ukubwa wa mita za mraba 710,000 kwa gharama ya shilingi Bilioni 24,na ujenzi wa mifereji yenye urefu wa jumla ya kilomita 100 kutoa maji mashambani;ujenzi wa nyumba mbili za watumishi na usanifu wa jengo la Umwagiliaji Mkoa,” alisema Katuta.Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Salum Kalli emahakikishia serikali kuwa serikali itahakikisha ulinzi wa Mradi na Kumshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Pamoja na waziri wa kilimo Hussein Bashe kwa kufikisha huduma ya Umwagiliaji katika wilaya ya Kigoma.

Akimkaribisha Waziri wa Kilimo, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye, ameishukuru serikali kwa uwekezaji Mkubwa unaofanywa katika Mkoa wa Kigoma, kupitia kilimo cha umwagiliaji.

“Kilimo cha umwagiliaji ni mühimu sana katika kuinua uchumi wa Mkoa wetu wa Kigoma kwani Mkoa wetu una zaidi ya hekta 100 zinazofaa kwa umwagiliaji lakini mpaka sasa ni hekta 9000 tu ndizo zinazo tumika,”amesema Andengenye.
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini Ngenda Shabani Kirumbe,amemshukuru raid Dkt Samia Suluhu Haasan kwa kufanikisha utekelezaji wa Mradi wa Luiche kwani kufanya hivyo kutawezesha kuongezeka kwa mzunguko wa fedha katika mkoa wa Kigoma.

“Tunamshukuru sana Rais Samia Suluhu Haasan kwa uwekezaji wa zaidi ya trilioni 3 katika Mkoa wetu wa Kigoma na kutupatia Bilioni 60 za utekelezaji wa Mradi wa Umwagiliaji Luiche.Kataeni watu wanao taka kuwarudisha nyuma kwa kuwadanganya kuwa mtapewa fidia kwa ajili ya kupisha ujenzi wa miradi ya miundo mbinu,”alisema Ngenda.
Mradi wa Luiche upo katika wilaya ya kigoma, mkoa wa Kigoma. Mradi huu unajumuisha vijiji vya Kamara, Simbo, Kaseke, Nyamori, Msimba, Matiazo pamoja na Kagera. Mradi huu utakuwa na ya hekta 3000 zitakazomwagiliwa baada ya ujenzi kukamilika. 

Mradi huu wa Luiche umegawanyika katika mikataba miwili ambayo ni Mkataba wa ujenzi wa bwawa pamoja na mkataba wa ujenzi wa skimu ya umwagiliaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news