Waziri Bashungwa azindua hoteli mpya ya Mlimani City Mikyolo

KAGERA-Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa (Mb) ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inyoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuboresha miundombunu ya barabara katika Wilaya ya Karagwe hivyo amewataka Wawekezaji na Wafanyabishara kuendelea kuchangamkia fursa za uwekezaji.
Bashungwa ameeleza hayo leo Julai 7, 2024 wakati akizundua Hoteli mpya ya Mlimani City Mikyolo iliyopo Kata ya Bugene, Wilaya ya Karagwe na kueleza kuwa Serikali inaendelea kuweka mazingira bora na wezeshi ili kuwezesha wawekezaji kuwekeza na kuzalisha ajira mbalimbali kwa Watanzania.
“Tunajionea jinsi Wilaya ya Karagwe inavyoendelea kukua kila siku hususani katika miundombinu ya barabara, kama mnavyofahamu kazi za ujenzi wa barabara ya Bugene - Nyaishozi kuelekea Benaco inaendelea kwa kasi, sambamba na hiyo tumeshampata mkandarasi wa kuanza ujenzi wa barabara ya Omurushaka - Kyerwa kwa kiwango cha lami,” ameeleza Bashungwa.

Bashungwa ameeleza kuwa barabara zinazojengwa zikikamilika zitasaidia Wilaya ya Karagwe kufungua fursa za kibiashara ambazo zitawezesha wananchi kutumia nafasi hiyo kukuza uchumi wao binafsi na pato la Taifa.
Aidha, Bashungwa ametoa wito kwa uongozi wa Hoteli ya Mlimani City Mikyolo kutoa huduma bora na nzuri kwa wateja wake ili kuwavutia wateja wengine ambao wataeneza sifa nzuri za hoteli hiyo pamoja na ukarimu wa Wanakaragwe.

Naye, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe, Wallace Mashanda ameeleza kuwa uwekezaji katika Wilaya ya Karagwe ni muhimu sana kwani Wilaya hiyo limepakana na Hifadhi za Mbuga za wanyama ya Chato - Burigi na Ibanda Kyerwa, hivyo uwepo wa Hoteli utaongeza idadi ya wataliii kufika na kutembelea hifadhi hizo.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Bugene, Mugisha Anselmu amemshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za miradi ya maendeleo ambapo amewapatia Shilingi Milioni 580 kwa ajili ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Omurushaka na kiasi cha Shilingi Milioni 260 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya Shule ya Sekondari ya Bugene.
Akisoma risala ya uzinduzi, Bw. Ezekia Anselmu ameeleza kuwa hoteli hiyo ina vyumba vya kulala vyenye hadhi ya juu, eneo la maegesho ya magari lenye usalama wa kutosha, bustani za kupumzikia na viunga vyenye hewa safi na tulivu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news