Waziri Jafo ataka jengo la wizara likamilike kwa wakati

DODOMA-Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo amekagua ujenzi wa jengo la Wizara hiyo katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma na kuwataka wakandarasi kuhakikisha unakamilika kwa wakati.
Akizungumza Julai 8, 2024 baada ya kukagua ujenzi huo, Waziri Jafo ameridhishwa na kazi inayoendelea na matarajio ifikapo Septemba 30, 2024 ujenzi uwe umekamilika.
"Niwatake wasimamizi wa ujenzi huu ambayo ni Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) wasimamie vizuri pamoja na mkandarasi kuhakikisha kazi unakamilika ndani ya muda uliopangwa, imani yetu itakapofika Septemba 30, 2024 sisi watumishi tuweze kuhamia kwenye jengo hili."
"Nimefarijika na mapokezi katika Wizara hii, jambo kubwa ambalo tumejiwekea malengo ni kuhakikisha mchakato wa majengo unakamilika katika hii awamu ya pili na watumishi wote wanahamia,"amesema.

Aidha,amewataka watumishi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa bidii na ushirikiano.

"Ili tuweze kufikia Malengo ya Wizara yetu lazima tufanye kazi kwa bidii na Ushirikiano Ili tuendelee kumsaidia Rais wetu Mhe Dk.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,"amesisitiza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news