LUSAKA-Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UN Tourism) Kanda ya Afrika, Bi. Elcia Grandcourt.

Kikao hicho kilimefanyika leo katika Hoteli ya Avani Victoria Falls Resort, Jijini Livingstone Zambia na kuhudhuriwa na Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kitaalam wa UN, Bw. Jaime Mayaki, Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Richie Wandwi pamoja na Afisa Utalii wa UN Tourism, Bi. Zineb Remmal.