Waziri Mhagama akabidhi vifaa tiba Kituo cha Afya Liganga

RUVUMA-Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb) amesema, Serikali kupitia Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) imejipanga kuboresha huduma za afya ili kuokoa vifo vya wajawazito na watoto wakati wa uzazi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bungena Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) wa Peramiho akikabidhi vifaa tiba kwenye mkutano wa hadhara kwa ajili ya kituo cha afya cha Liganga katika ziara yake iliyofanyika kwenye kijiji hicho.

Kauli hiyo ameitoa Julai 9, 2024 wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika Kata ya Liganga iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.

"Kituo cha Afya Liganga kimepata vifaa tiba vienye thamani ya shilingi milioni 300 na hivyo kusaidia kuanza kutoa huduma za mabara na kupunguza adha ya wananchi kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.”
Ameelekeza wataalamu kuhakikisha wanaratibu vyema mipango ya kuunganisha kituo hicho na nishati ya umeme ambayo inatarajiwa kuunganishwa ifikapo mwishoni mwa mwezi wa saba.

Waziri Mhagama ametumia nafasi hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kusogeza huduma za afya karibu na wananchi na kuhakikisha zinafanya kazi vizuri.
Dkt. Rashid Mfaume Mkurugenzi wa huduma za afya ustawi wa jamii na lishe kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Liganga.

Awali Dkt. Rashid Mfaume Mkurugenzi wa huduma za afya, ustawi wa jamii na lishe kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI amemshukuru Waziri Mhagama kwa kuendelea kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Peramiho.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bungena Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) wa Peramiho akizungumza na Diwani wa Kata ya Liganga Mhe. Filbert Soko wakati wa ziara yake katika kata hiyo.

“Jitihada za Mbunge kuomba vituo vya afya vifaa tiba na hospitali zimesaidia sana kuboresha huduma za afya jimbo la Peramiho ambapo kwa mwaka uliopita wa fedha nyingi zilikuja Halmashauri ya Wilaya ya Songea,” amesema Dkt.Mfaume.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bungena Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) wa Peramiho akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wake walipotembelea katika shule ya msingi Mbolongo kujionea ujenzi wa vyumba vya madarasa.

"Waziri anapambana kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya, na hizi ni jitihada kubwa ambazo zinapaswa kupongezwa."
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bungena Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) wa Peramiho akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Ofisi ya Rais TAMISEMI wakati wa ziara yake kata ya Liganga.

Ameongeza kuwa, zoezi la kukabidhi vifaa tiba ni ishara tosha kwamba kituo cha afya Liganga kitatoa huduma zote zinazopaswa kuwepo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news