Waziri Mhagama awakumbushia wazazi

RUVUMA-Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Jenista Mhagama ambaye ni Mbunge wa Peramiho amehimiza wazazi kuongeza ukaribu na usimamizi mzuri wa malezi kwa watoto ili kujua mienendo yao ya makuzi na kuwaepusha na makundi rika yenye ushawishi mbaya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akijumuika kucheza ngoma na wananchi waliojitokeza kumlaki wakati wa ziara yake jimboni Peramiho.

Waziri ametoa kauli hiyo Julai 7,2024 wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea Vijijini mkoani Ruvuma ambapo amefanya mikutano niwili ya hadhara katika Kijiji cha Kizuka na Kitongoji cha Ligunga.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho akikagua Ujenzi wa Miundo mbinu ya Maji Safi katika Shule ya Msingi Ligunga Halmashauri ya Songea mkoani Ruvuma.

“Vitendo vibaya vya udhalilishaji wa watoto vinafanyika mtaani, hivyo ni vyema tukawa tunafanya ukaguzi kwa watoto ili kujiridhisha usalama wao ikiwa ni pamoja na kufuatilia mabadiliko yao,” amesema Waziri Mhagama.
Amefafanua kwamba watoto ni baraka kutoka kwa Mungu, tuilinde baraka hiyo tuliyopewa na Mungu kwa kuzungumza nao kila wakati kuhusu makuzi yao.

"Ukiona mtoto wako wa kiume na wa kike ana mabadiliko ni vyema kufanya ufuatiliaji haraka kwa sababu tuna binadamu wenye mioyo na tabia za unyama na hawaoni dhambi kuharibu watoto wa wenzao."
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu),Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akifurahia jambo na Wanafunzi wa shule ya msingi Ligunga alipotembelea kujionea ujenzi wa miundo mbinu ya maji, madarasa na matundu ya vyoo.

Katika hatua nyingine Waziri Mhagama ameendelea kuhimiza vijana kuepukana na uraibu wa matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo bangi, ameeleza kwamba vitendo vyote visivyo na maadili hufanyika kutokana na ushawishi wa madawa ya kulevya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akikagua maendeleo ya ujenzi wa tenki la maji lenye uwezo wa kujaza lita 150,000 katika kijiji cha Kizuka.

“Wale wote ambao jamii inaona wameingia kwenye uraibu wa dawa za kulevya toeni taarifa ili waweze kupelekwa kwenye vituo vya utengamao vitakavyowasaidia kuachana na matumizi ya dawa za kulevya,”amesema Waziri Mhagama.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Songea Vijijni, Thomas Masolwa akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu),Mhe. Jenista Mhagama (Mb) na Mhandisi wa TARURA wilaya ya Songea Vijijini Simoni Binamu (aliyesimama) katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika kitongoji cha Ligunga.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Songea Vijijini,Mtela Mwapamba ametoa rai kwa wananchi kuendelea kujitokeza kufuatilia vyeti vya kuzaliwa vya watoto ili viweze kuwasaidia pindi inapotokea uhitaji wa kutumia kwa shughuli mbalimbali.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akigawa vifaa vya michezo kwa timu mbalimbali wakati za ziara yake katika Kijiji cha Kizuka Halmashauri ya wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.

“Sio mpaka mtoto amefaulu kwenda kidato cha kwanza, au anatakiwa kwenda Jeshi la Kujenga Taifa ndio mzazi unaanza utaratibu wa kutafuta cheti hiyo sio sawa lazima tuwe na vyeti vya vijana wetu mapema,” amesema Mwapamba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news