Waziri Mhagama awasha umeme Chihurungi

RUVUMA-Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Jensita Mhagama ametaka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuhakikisha wanaweka mkakati mzuri wa kusaidia kusambaza umeme vijijini kwa taasisi za Serikali na dini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akiwasha umeme katika Kitongoji cha Shuleni kilichopo katika Kijiji cha Chihurungi Halmashauri ya Songea Vijijini.

Waziri ametoa kauli hiyo Julai 14,2024 wakati wa hafla ya kuwasha umeme katika Kitongoji cha Shuleni Kijiji cha Chihurungi kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.

"Halmashauri yetu sasa imebakiza vijiji vinne, na vijiji venyewe mpaka mwezi wa tisa mwaka huu, vijiji vyote vitakuwa vinawaka umeme ikiwemo Kijiji cha Nambendo kilichopo pembezoni ambacho tayari utandazaji wa nyaya za umeme unaendelea.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu),Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akizungumza na wananchi wa Chihurungi na Parangu wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo.

"Tunao moyo wa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, huku tukiendelea kuomba vitongoji vilivyoongezwa kuwekewa umeme vipate umeme haraka.

"Wananchi wa Chihurungi umeme huu mkautumie vizuri ili kuleta faida fungamanishi za kiuchumi, ikiwemo viwanda vya chuma, na viwanda vya kutengeneza magrili,"alifafanua.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa (REA) wakati wa hafla ya kuwasha umeme katika Kitongoji cha Shuleni kilichopo Kijiji cha Chihurungi.

Awali Wakala wa Nishati Vijijini na Msimamizi wa Mradi wa (REA) Mkoa wa Ruvuma,Mhandisi Robert Ndule amesema, Chihurungi ni moja ya vijiji 28 vilivyokuwa vimebaki kupatiwa umeme katika Halmashauri ya Songea Vijijini.

“Kijiji hicho kina wigo wa wateja 64 na kwa sasa kimeunganisha wateja tisa, hivyo tunaendelea kutoa wito kwa taasisi za Serikali na zisizo za Serikali kutuma maombi ya kuunganishwa,”amesema Mhandisi Ndule.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Songea, Mtela Mwampamba akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Parangu na Chihurungi.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Songea,Mtela Mwampamba amegusia umuhimu wa wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya pamoja kwa familia mfuko ambao unajumuisha watu sita kutibiwa kwa mwaka mzima.

"Ukiwa na bima ya afya inasaidia kupata huduma za afya pindi magonjwa yanapojitokeza ghafla na ukiwa hauna fedha, hivyo tutumie fursa hii tuliyonayo wakati wa mavuno kujiunga na bima ya afya."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news